WANANCHI KUPATA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU KWA NJIA YA KISASA ZAIDI

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe samia suluhu hassan amesema serikali itaendelea kuweka mazingira bora yatakayosaidia wananchi kupata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi.
Mhe samia akifungua mkutano wa mwaka wa chama cha kampuni za simu duniani jijini dar es salaam amesema anaimani kuwa wadau hao watajadili namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa na kuwafikia wananchi wengi hasa maeneo vijijini ambapo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.
Aidha ameleeza kuwa kwa sasa tanzania ni miongoni mwa nchi kusini mwa bara la afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki.
Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia profesa makame ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na kampuni za mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na ubora unaotakiwa.