WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA TAFITI

Wananchi wanahitajika kutoa mashirikiano kwa wadadisi wa utafiti wa awanu ya pili wa kutathmini matokeo ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini tanzania ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa mipango ya nchi.
akizungumza na zbc katika mazoezi ya vitendo ya upimaji wa watoto juu ya utekelezaji wa zoezi hilo katika hospital ya mwembeladu afisa utafiti wa taasisi ya lishe kutoka daresalaam nd sauli epimack amesema utawezesha kutambua afya za watoto na changamoto zao za makuzi.
Amefahamisha kuwa lengo la uchukuwaji wa vipimo kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 ili kutathmini hali ya hali ya lishe nchini kupitia mpango wa kuzinusuru kaya masikini tanzania.
Mratibu wa utafiti huo bi asiya takrima amesema hali ya zoezi hilo linakwenda vizuri kutokana na kutolewa vizuri kwa taaluma kwa wadadisi wa zoezi hilo pamoja na kukamilika kwa vifaa kunakopelekea kufanyika kwa wakati .
Wadadisi wa zoezi hilo wameomba kupewa ushirikiano zaidi wakati wa upimaji wa watoto hao ili kuwezesha kupatikana vipimo stahiki kwa manufaa ya mipango ya maendeleo ya watoto nchini.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmin mwezi ujao litazihusisha zaidi ya kaya 2040 katika shehia 90 zilizomo katika mpango wa kunusuru kaya masikini unguja na pemba .