WANANCHI KUTUMIA FURSA YA KUPIMA AFYA ZAO

 

Wananchi wametakiwa kutumia fursa ya kupima afya zinazotolewa na wizara ya afya katika kupima afya zao ambazo huduma hizo huwafikia moja kwa moja kupitia shehia zao.

Daktari dhaman a wa wilaya ya mjini ramadhan mikidadi akizungumza katika upimaji afya uliofanyika skuli ya kidongochekundu amesema mpango huo ni muendelezo wa ziara ya afya kutoka huduma katika wilaya zote za zanzibar kupitia shehia.

Miongoni mwa huduma zilizotolewa ni upimaji wa koo, masikio, sukari na macho ambapo zoezi hilo limejumuisha wakaazi wa shehia za jang’ombe, kidongochekundu na matarumbeta huku viongozi wa shehia wakiomba huduma hizo ziwe endelevu.

Wananchi waliojitokeza wameelezea kufurahiswha na mpango huo wa wizara ya afya kutoa huduma hizo bila ya malipo.