WANANCHI KUTUMIA VITUO VILIVYOKARIBU YAO ILI KUWAPA NAFASI MADAKTARI BINGWA KUFANYA UTAFITI

 

Waziri wa afya mh hamad rashid mohammed amewataka wananchi kutumia vituo vilivyokaribu yao ili kuwapa nafasi madaktari bingwa kufanya utafiti wa maradhi makubwa katika hospitali ya mnazi mmoja.Wakichangia hutuba ya makadirio na mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ya ofisi ya makamo wa pili wa wamesema maradhi hayo yamekuwa yakiwapa hofu wananchi wengi kutokana na kuwashambulia.

Wamesema taarifa  hiyo ya serikali itasaidia wananchi hao kuchukuwa tahadhari ya kuweza  kujikinga na maradhi hayo.Kuhusu huduma za watu wenye ulemavu  hospitali wajumbe hao wamesema kumekuwa na tatizo kubwa ikiwemo uhaba wa dawa na viungo bandia pamoja na ukosefu wa vifaa vya kusomea wanafunzi hali inayopelekea kutofanya vizuri katika mitihani yao na kuzoretesha maendeleo yao