WANANCHI KUVAMIA MAENEO YA CHUO CHA KIISLAMU KWA SHUGHULI ZAO BINAFSI.

 

Mkuu wa chuo cha kiislam dr. Muhidin Ahmad,   amelalamikia tabia inayoendelea kwa baadhi ya wananchi kuvamia maeneo ya chuo hicho kwa shughuli zao binafsi.

Amesema tabia hiyo inayoendelea inatokana na kukosekana kwa uzio katika eneo la chuo jambo ambalo limekuwa likiwafanya wananchi kuingia ovyo katika maeneo hayo.

Hayo yamebainika baada ya  zbc kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa kuwachaguwa viongozi wa  serikali ya wanafunzi chuo hicho, na kuzungumza na mkuu huyo dr. Muhdin ambapo amesema sababu kubwa inayochelewesha kujenga uzio, ni ukosefu wa hati miliki  wa eneo hilo.

Mshauri wa chuo hicho dr. Ali ame na mlezi wa serikali ya wanafunzi mwalim juma ,wamesema wamekuwa wakiwasimami wanafunzi katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya serikali na ya upande wa elimu ipasavyo bila ya kuvunja sheria na maadili ya chuo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa chuo cha kiislam, seif sleiman amemtangaza nd. Issa taib kuwa mshindi wa urais wa serikali ya wanafunzi kwa kupata kura 316 sawa na asilimia 59.8.

Akitoa neno la shukurani rais huyo amesema atatekeleza matatizo yanayokikabili chuo hicho.