WANANCHI KUVITUMIA VIKUNDI VYA USHIRIKA SACOSS KWA LENGO LA KUJILETEA MAENDELEO

Wananchi wametakiwa kuvitumia vikundu vya ushirika sacoss kwa lengo la kujiletea maendeleo na sio manbo mengine yasiyokuwa na faida yoyote.
akizungumza na wanakikundi cha ushirika wa maendeleo kidongo chekundu umaki sacoss .mbunge wa jimbo la jang’mbe ali hassan king amesema ni vyema wanakikundi hao wajiekee malengo maalum ili waweze kufika mahali wanapohitaji.
Pia amewataka wanaushirika hao kuwa na subra na kuwahakikishia atakuwa nao bega kwa bega katika shuhuli zao kwani mafanikio watakayoyapata ni mafanikio ya taifa kwa ujumla.
Mgeni rasm katika hafla hiyo ya umaki saccos inayotimiza miaka 10 ikiwa na wanachama 148 waziri wa biashara,viwana na masoko mh balozi amina salum ali amesema wananchi wanatakiwa kuendeleza miradi mbalimbali hususan katika vikundi vya ushirika kwani ni njia moja wapo ya kujikwamua na janga la umasikini.
Nao miongoni mwa wanakikundi hicho wameeleza mafanikio ambayo wameyapata pamoja na changamoto mbalimbali na kutoa ushauri kwa wananchi wengine kuanzisha vikundi vya ushirika katika kujikwamua kiuchumi.