WANANCHI KUZITUMIA KAMATI ZA SHEHIA YANAPOKEA MAFAA KATIKA MAENEO YAO.

Kamisheni ya kukabiliana na maafa zanzibar imewataka wananchi kuzitumia kamati za shehia yanapokea mafaa katika maeneo yao.
Mkurugenzi mtendaji wa kamisheni hiyo shaaban seif mohammed amesema hao watu wanatambulika na wananweza kufikisha taarifa za kuchukuwa hatua za haraka hadi katika ngazi ya kitaifa.
Akizungumza alipowatembelea waliopata maafa ya upepo katika maeneo ya mahonda mto mchanga amesema nyingi ya nyumba zilizoathirika hazikuzingatia vigezo vya ujenzi hali iliyochangia maafa hayo.
Baadhi ya watu ambao nyumba zao zimeathiriwa na upepo huo amesema hatua ya kutembelewa na kufanyiwa tathmini ya maafa hayo inawapa faraja ya kuona jinsi serikali inavyoweza kuwasaidia.