WANANCHI WA DIMANI WAMETAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA ZA UWEKEZAJI WA MAENEO YA ARDHI

 

 

mkuu wa wilaya ya maghari b kepten silima haji haji  amewataka wananchi kufuata taratibu za  kisheria za uwekezaji wa maeneo ya ardhi ili kuepusha migogoro isitokee.

wito huo ameutowa alipofanya ziara ya kutembea eneo linalodaiwa   kuvamiwa na wawekezaji ambao hawajulikani  kisheria  kwa lengo la kujenga kiwanda cha matofali huko shehia dimani eneo la chomoani wilaya ya magharibi b.

amesema endapo wananchi watafuata taratibu za kisheria za uwekezaji kwa kufika katika mamlaka inayohusika na masuala ya uwezekezaji (zipa) migogoro ya ardhi itapungua na kuweza kupatiwa taratibu zinazofaa ili kuendelea na shughuli za kimaendeleo.

aidha amesema eneo hilo ni umiliki wa mamlaka ya maji zanzibar zawa hivyo amesitisha kutotumiwa kwa eneo hilo hadi mamlaka husika iweze kutoa taratibu za kisheria zinazohusika.

nae wa shehia hiyo nd. khatibu ame bakari amesema eneo hilo linasemekana ni eneo la muekezaji ambae hajulikani kisheria na serikali hivyo eneo hilo kwa sasa linamilikiwa na mamlaka ya maji zawa ambapo linavisima vya maji vya mamlaka hiyo.