WANANCHI WA KIKUNGWI KUOMBA KUPATIWA SOKO LA UHAKIKA BADALA YA KUKAA KANDO YA BARABARA.

 

 

Wananchi wa kijiji cha kikungwi wanaojishughulisha na biashara ya chaza wameiomba serikali na viongozi wao wa jimbo kuwatafutia eneo litakalowawezesha kupata soko la uhakika badala ya kukaa kando ya barabara.

wakizungumza katika kikao cha kukabidhiwa vitendea kazi wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa wanafanya biashara zao kando mwa barabara hivyo wanahitaji sehemu maalum itakayowawezesha kufanya kazi zao kwa usalama.

mwakilishi wa jimbo hilo Mh: Simai Muhammed amewataka wafanyabiashara hao kuvitumia vyema vifaa walivyopatiwa na wanaendelea na juhudi za kuwatafutia sehemu ya uhakika itatayowawezesha kufanya biashara zao.

mkurungezi wa safari blue Bi Eleanor Griplas amesema ni jambo zuri kuona akinamama wanajishughulisha na biashara za kujiendeleza kiuchumi na kuahidi kuwasaidi katika biashara zao.