WANANCHI WA KISIWA CHA TUMBATU WAMESHAURIWA KUEZEKA MAPAA YA NYUMBA ZAO

 

Wananchi wa kisiwa cha tumbatu wameshauriwa kuezeka mapaa ya nyumba zao kwa tindo ambao utaweza kuhimili upepo licha ya vipato vyao kuwa vya chini.Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa kamisheni ya kukabiliana na maafa bw. Makame khatib makame wakati walipofika kijijini hapo akiwa ameongozana na watendaji wenzake kwa ajili ya kufanya tathmini pamoja na kuwapa mkono wa pole wananchi waliopatwa na maafa kufuatia upepo mkali ulioathiri nyumba za makaazi zipatazo mia moja na thalathini na sita (136) shehia zilizoathiriwa upepo huo ni shehia ya tumbatu uvivini ambapo kuna jumla ya nyumba ishirini na moja (21), shehia ya tumbatu gomani nyumba hamsini na sita (56) ikiwemo madrasa ya kur-ani  na shehia ya tumbatu mtakuja nyumba hamsini na tisa (59).

Jumla ya athari zilizojitokeza kufuatia upepo huo ni pamoja na watu sita kupata majaraha kwa kuangukiwa na matofali ya nyumba pamoja na kukatwa na mabati, nyumba kuezuka mapaa pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme.Nae mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini “a” bw mussa ali makame amewataka wananchi waliofikwa na maafa hayo kuwa na moyo wa subra pamoja na mashirikiano hasa katika kipindi hichi kigumu na kuahidi kua suala hilo watalifanyia kazi kwa mashirikiano ya kamisheni ya kukabiliana na maafa.Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliopatwa na maafa haya ya upepo mkali bibi sauda haji mwadini ametoa neno la shukurani kwa watendaji waliofika kuwafariji kufuatia tukio hilo.