WANANCHI WA KUSINI KUFUATA SHERIA PAMOJA NA MIONGOZO INAPOTOLEWA NA SERIKALI

 

Mkuu wa wilaya ya kusini ndugu idrissa kitwana mustafa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufuata taratibu sheria pamoja na miongozo inapotolewa na serikali ili kujiepusha na mambo yasiyo ya lazima.

Wito huo ameutoa nichamvi alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliokataa kupigiwa dawa za majumbani .

Ndugu kitwana amesema kuwa serikali ya mapinduzi zanzibar inatumia fedha nyingi kwa kuwahudumia wananchi wake kuepukana na maradhi mbali mbali ikiwemo maleria .

Pia amewataka wananchi kuacha visingizio visivyo na sababu  kwa kukataa zoezi hilo na kusema kuwa serikali ya wilaya haitomvumilia mtu yoyote atakae kaidi amri ya serikali.

Jumla ya nyumba 253 ambazo zilikataliwa kupigwa dawa hizo zimepigwa chini ya usimamizi wa mkuu wa wilaya hiyo.