WANANCHI WA SHAKANI WAMELALAMIKIA HALI YA UCHIMBAJI WA KIFUSI UNAOFANYWA NA MFUGAJI WA SAMAKI

Wananchi wa shehia ya shakani wamelalamikia hali ya uchimbaji wa kifusi unaofanywa na mfugaji wa samaki katika maeneo hayo bila ya wenyeji wa hapo kushirikishwa.
Wamesema kazi ya ufugaji wa samaki unaofanywa na kijana huyo haunapingamizi kwao ila wanachokilalamikia ni kitendo cha kuchimba kifusi na kusababisha kuongeza mashimo zaidi kuliko yale aliyoruhusiwa kufugia samaki bila ya kuushirikisha uongozi wa shehia hiyo.
wamelalamika kwa kusema kijani huyo amekuwa akichimba kifusi kwa manufaa yake mwenyewe na kukiuza kitendo ambacho kinaweza kusababisha hali ya kutokuwa na maelewano hapo baadae.
Sheha wa shehia ya shakani mwanaisha khamis rashid amesema vitendo hivyo vinasababisha mashimo mapya zaidi ya yale aliyoruhusiwa kufuga samaki kwa maslahi yake mwenyewe.
Mkuu wa wilaya ya magharibi b silima haji wa haji amesema mradi wa ufugaji wa samaki uliobuniwa na mwekezaji huyo ni mzuri ila alichomshauri kwamba ni vyema akafuata utaratibu pamoja na kushirikiana na wanakijiji hao.
zbc ilifanikiwa kumpata mfugaji huyo anaejulikna kwa jina la saidi ibrahim abdalla mkaazi wa shehia ya shakani na kuwataka wakaazi hao kumpa nafasi ya kujiimarisha zaidi ili baadae wananchi na wao waweze kunufaika.