WANANCHI WA SHEHIA YA MUNDULI HAWAPATI MAJI KWA UHAKIKA

 

Licha ya juhudi za kuimarisha huduma  ya  maji  safi  na  salama  nchini bado  wananchi wa shehia ya munduli hawapati maji kwa uhakika hali inayowafanya kuyatafuta muda mwingi na hivyo kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo.

Wananchi hao wameiomba  serikali kupitia viongozi  wa  jimbo  kuweka  mkazo   kuimarisha  upatikanaji wa huduma  hiyo ambayo ni muhimu kwa maisha ya viumbe vyote ulimwenguni.

Wamesema waathirika wakubwa wa tatizo hilo ni wanawake na watoto ambao mara nyingi hubakia majumbani hivyo hakuna budi serikali ikawangalia kwa jicho la huruma  ili waondokane na shida hiyo.

Diwani  wa  wadi  yamunduli  nd juma  fikirini  alivyofika  kusikiliza  malalamiko  yao  amesema ipo  haja  kuwepo  kwa  utaratibu   mzuri wa kusambaza maji kutoka katika    visima  ili maji  yawafikie wananchi wa maeneo yote.

Wakati  huo  huo  diwani  huyo  alitembelea skuli ya mtopepo kuangalia   ukarabati  wa  vyoo  vya  skuli  ya  mtopepo

Mwalimu  wa skuli  hiyo  bi  salma  ahmada  amesema   licha  ya  ukarabati  unaofanyika  wa  vyoo  hivyo  bado  nguvu   inahitajika  kuengezwa    kutokana  na idadi  kubwa  ya  wanafunzi  iliopo  katika  skuli  hiyo.