WANANCHI WA SHEHIA YA TUMBE KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTATUA MGOGORO WAO

 

Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa shehia ya tumbe wilaya ya micheweni kuunda kamati maalumu ya kutatua mgogoro wao na halmashauri kuhusu mgao wa fedha za soko hilo.

Amesema iwapo wananchi hao watashindwa kumaliza  mgogoro huo serikali itafanya maamuzi rasmi kuhusu  matumizi ya fedha hizo kwa shughuli nyengine.

Balozi Seif ametowa wito huo ndani ya soko hilo baada ya kutembelea meneo tofauti na kupata maelezo juu ya wananchi kususa kulitumia soko hilo ambalo lilifunguliwa Januari 2015 na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Amesema serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza katika eneo hilo ikiwa na lengo la kuwapa fursa wavuvi na wananchi kuendesha biashara zao katika eneo la kisasa bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Wakitowa maelezo juu ya mgogoro wa soko hiloMkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mh. Omar Khamis Othman, Mkuu wa wilaya ya Micheweni Abeid Juma wamesema.

Mapema akitembelea eneo la Shumbamjini ambalo linatarajiwa kujengwa bandari rasmi na kusema kuwa yeye binafsi amewafiki kujengwa kwa bandari hiyo kwani anaamini kutakuwa na miundombinu bora ya bandari itakayozingatia usalama wa wananchi na mali zao.

Akitowa maeelezo ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Shomari Omar Shomari na Mkurugenzi wa huduma za bandari Hassan Mohamed wamesema eneo hilo lina kima cha maji cha kutosha na litatowa fursa vyombo vingi kuweka nanga katika eneo hilo.

Kwa upande wa wananchi wa Shumbamjini wameipokeaje suala la kujengwa bandari katika eneo hilo.