WANANCHI WA VIJIJI VYA UKANDA WA PWANI WAMETAKIWA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII

Wananchi wa vijiji vya ukanda wa pwani katika mkoa wa kusini unguja wametakiwa kuimarisha sekta ya utalii na kukuza uchumi wa taifa kwa kudhibi wimbi wa wahamiaji holela ndani ya vijiji vyao.
Akizungumza katika ofisi ya mkoa tunguu katibu mtendaji kamisheni ya utalii zanzibar dk vuai idd lila katika kikao cha pamoja kilichowashirikisha watendaji wa kamisheni hio, maofisa wa jeshi la polisi na watendaji wa afisi ya mkoa chenye lengo la kutafuta namna ya kudhibi vitendo vinavyohatarisha usalama wa watalii na mali zao.
Dr. Lila amesema pamoja na jitihada za kamisheni hiyo katika kuimarisha usalama wa wageni lakini bado kumeonekana kuendelea kujitokeza kwa baadhi ya matukio kufanyiwa watalii wanaoingia nchini ikiwemo kwa kubughudhiwa na mapapasi, kuporwa mali zao, kuongezeka kwa wimbi la uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya katika fukwe jambo ambalo linapelekea kwa baadhi ya wageni kuchukizwa na tabia hizo na kuondoka nchini.
Nae mkuu wa mkoa wa kusini unguja mhe hassan khatib hassan amesema serikali ya mkoa kwakushirikiana na jeshi la polisi mkoani humo litahakikisha kwamba linachukuwa hatua za makusudi za kuwadhibiti watu wanaoingia kinyume na taratibu za serikali zilizowekwa katika kuendelesha shughuli za kitalii kwenye maeneo ya fukwe.
Aidha amesema ili kutekeleza azma ya serikali ya utalii kwa wote juhudi za kuwaelimisha wananchi wa ukanda wa pwani zinahitajika juu ya dhana hiyo ili kuona kwamba sekta hio inaimarika nakuwanufaisha wananchi wa vijiji hivyo.
Kwa upande wa mkuu wa dawati la utalii makao makuu ya polisi zanzibar nd hamid haji amesema jeshi la polisi tayari limeshapanga mikakati ya kukabiliana na vitendo hivyo katika mikoa yote ya zanzibar.