WANANCHI WA ZANZIBAR WAMEUPONGEZA UAMUZI WA SERIKALI WA KUZIMWA KWA MFUMO WA ANOLOGIA

Wananchi wa Zanzibar wameupongeza uamuzi wa serikali wa kuzimwa kwa mfumo wa anologia kwa shirika la utangazaji zanzibar ZBC na kuendelea kurusha matangazo yake kupitia Digitali ili kuendana na mabadiliko ya teknologia yaliopo ulimwenguni

Wakizungumza na ZBC wananchi hao wamefahamisha kuwa dunia kwa kipindi hichi imefanya  mageuzi makubwa katika nyanja za mawasiliano hivyo zainzibar kuondoka katika utaratibu huo ni hatua muhimu.

Hata hivyo wananchi hao wameitaka kampuni inashughulika na masuala ya  ving’amuzi Zanzibar, (ZMUX)  kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa kuwa wananchi wengi wa zanzibar wanatarajia kutumia huduma hiyo kutoka kwao.

akizungumza na ZBC msaidizi afisa teknolojia ya habari na mawasiliano   ZMUX  adil  ali  saleh,  amesema     mageuzi hayo yatawawezesha wananchi kupata channel zaidi ya moja kwa kutumia ving’amuzi vya kisasa vyenye  uwezo wa hali ya   juu.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji Zanzibar Imane Duwe amesema mabadiliko ya Teknolojia yataweza kuwasaidia waandishi wa habari wa ZBC katika kuongeza uelewa wa masuala ya habari duniani.

Kupitia shirikla la utangazaji zanzibar  kauli  ya  waziri wa habari utamaduni utalii na michezo mh rashid ali juma,ametangaza rasmi kwamba  ifikapo mwishoni mwa mwezi wa agosti shirika la utangazaji zanzibar zbc litazima   mitambo yake ya analogi  na kuanza kurusha matangazo hayo kwa njia ya dijitali