WANANCHI WALIOMO KATIKA MPANGO WA KUZINUSURU KAYA MASIKINI WAMEPATA MABADILIKO MAKUBWA YA KIUCHUMI

 

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mh. Mohamed Aboud Mohamed amesema wananchi waliomo katika mpango wa kuzinusuru kaya masikini wamepata mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

Amesema mabadiliko hayo yamekuja kutokana na ruzuku wanazozipata kuziwekeza katika shughuli za uzalishaji na nyengine katika huduma za elimu na afya.

Waziri aboud amesema hayo wakati akizungumza na zbc baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya wananchi waliokatika mpango wa kuzinusuru kaya masikini kupitia tasaf awamu ya tatu wa shehia ya mlindo wilaya ya wete.

Amesema dhamira kubwa ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni kuwaondoa watu kwenye umasikini kwa kuwawezesha ili waweze kuyamudu maisha ya kila siku.

Sambamba na hili mh. Aboud amesema wananchi huzitumia ruzuku katika miradi mikubwa ya huduma za kijamii ili kujiondoshea usumbufu wa upatikana wa huduma ikiwemo mradi wa maji sahi na salama, barabara ambayo ni mafanikio ya taifa.

Akizungumza suala la changamoto alizogundua katika ziara hiyo, amesema tayari wameshafanya tahmini ya tasaf amuwa ya tatu na kitakachofuata ni tasaf awamu ya tatu ya pili ili kuzipatia ufumbuzi changamoto za wakaya hao.

Nao wakaya walio katika mpango huo hawakucha kuishukuru smz kwa kuwapatia ruzuku hizo na wameomba mradi huo uendelee kwani unawasaidia katika huduma za watoto.

Kaya alizozitembelea waziri aboud kiwanda cha uchongaji, uuzaji wa duka, uzalishaji wa majani ya chain a ushonaji katika shehia ya mlindo wilaya ya wete.