WANANCHI WAMEIOMBA SERIKALI KUYAFANYIAKAZI HARAKA MIUNDOMBINU YA PITAYO MAJI

Wananchi    wameiomba  serikali  kuyafanyiakazi  haraka  miundombinu  ya  pitayo  maji  mvua   ili  kuweza  kuwanusuru  wakaazi wa  maeneo  ya  mabondeni  na  mvua  za  masika  zinazotajiwa  kunyesha  hivi  karibuni.

Wakizungumza  na  zbc  wakaazi  wa  maeneo  ya  bububu  ,  mpendae  kwabiti  hamrani  wamesema  wanaishukuru  serikali  kwa  maandalizi  ya  ujenzi  wa  mitaro  mikubwa  ipitayo  maji  kwani  kufanya  hivyo  kunawezesha  kutatua  changamoto  hiyo   kwa kila  nyakati  za  mvua  zinapowadia.

Wamesema   kuitekeleza  amri  ya  serikali  kuhama  maeneo  hayo  inawawia  vigumu  kutokana na  ukosefu  wa  makaazi  hivyo  wameiomba  serikali  kuiharakisha  miundombinu  iweze  kukidhi  kina  kikubwa  cha  maji  ili  kuweza  kubaki  maeneo  yao  pasi  na  uharibifu  wowote  kutokea katika  maeneo  yao.

Imekuwa  ni  utaratibu   kwa  wananchi kupewa  hifadhi  ya  makaazi  kwa  kila  msimu  wa  mvua  za  masika  zinapowadia  kutokana na  athari  zinazowapata  wakaazi  wa  maeneo  ya  mabondeni  kwa  kukabiliwa  na  maafa  tofauti  ikiwemo  uharibifu  wa  mali  na  vifo  kwa  watoto kutokana  na  kuingiliwa na mali katika  makaazi  yao.

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App