WANANCHI WAMEISHUKURU SERIKALI KWA UJENZI WA BANDA LA KUSUBIRIA WAGONJWA

Wananchi Kutoka Maeneo Mbali Mbali Wameishukuru Serikali Kupitia Wizara ya Afya kwa Ujenzi wa Banda la Kusubiria Wagonjwa Katika Hospitali Kuu ya Mmnazi Mmoja.

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti Wananchi Hao Wamesema Kumalizika kwa Ujenzi Huo Kutawawezesha Kukaa Katika Eneo Yenye Stara Tofauti na Sasa Ambapo Wanakaa Sehemu Yoyote Wakisubiri Muda wa Kuangalia Wagonjwa.

Akizungumza na Zbc Msemaji wa Hospital  Hiyo Hassan Makame Mcha   Amesema Wamelazimika Kujenga Banda Hilo Kutokana na Malalamiko ya Wananchi Wanaokuja Kusubiri Wagonjwa wao Ambao Hulazwa  katika Hospitali Hiyo Ambapo Wengi wao Wanatoka Maeneo ya Nje ya Mji.

Amesema ujenzi huo utakapo Malizka Kutakuwa na Maeneo aalum ya Kulala Watu wanaosubiri wagonjwa wao na kuondoka na hali iliyopo hivi sasa kulala katika wodi wakati unapokuwana wagonjwa.

Amesema Ujenzi Huo Unatarajiwa Kumalizika Mwezi Ujao Umegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 30 na Utachukua Wananchi Zaidi ya 150.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App