WANANCHI WAMEITAKA SERIKALI KUWAJENGEA ENEO LA KUWASUBIRIA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA

 

Wananchi wanaosubiria wagonjwa wao hospital ya mnazi mmoja katika majengo ya dodoma wameiyomba serikali kuwaekea eneo maaluma la kusubiria wagonjwa kwani wamekuwa wakipata taabu wakati wanapoleta wagonjwa wao.

Wakizungumza na zbc tv wananchi hao wamesema mazingira ambayo wanakaa katika kusubiri wagonjwa wao sio mazuri na wala haridhishi lakini inawalazimu  wakae kutoka na kusubiria wagonjwa wao.

Aidha wamesema eneo ambalo limewekwa kusubiria wagonjwa liko mbali na walikolazwa wagonwa wao hali ambayo italeta usumbufu wakati  wanapohitajika

Akizungumzia kuhusu suala hilo msemaji wa hospital hassan makame mcha amesema sehemu ambayo wanakaa wananchi hao sio sahihi katika kusubiri wagonjwa kwani wizara imetenga eneo maalum   ambalo wananchi wanatakiwa kukaa na kusubiri wagonjwa wao.

Asemema wizara itachua hatua ya kuwaondosha wale wanaokaa  katika eneo hilo kwani sio salama kukaliwa na wananchi pia haliteti sura mzuri katika mazingira ya hospital.