WANANCHI WAMENUFAIKA NA HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA NA JUMUIYA YA WATANZANIA

Wakaazi wa vijiji vya mahonda na bumbwini wilaya ya kaskazini b wamenufaika na huduma za afya zilizotolewa na jumuiya ya watanzania wanaoishi nje dayaspora na jumuya ya noah ya kutoka korea ya kusini.
Taasisi hizo zimetoa huduma ya uchunguzi na matibabu kwa maradhi mbalimbali ikiwemo ngozi, macho, maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ambapo kiasi ya watu elfu moja wamepatiwa matibabu.
Mmoja wa madktari wa jumuiya ya diaspora jasmini rubama amesema lengo la kuwasaidia watanzania kupata huduma kwa za afya kwa ukaribu na kuwasisitiza wananchi kufuatilia huduma hizo.
Daktari dhamana wa wilaya ya kaskazini” b” daniel pius amesema huduma hizo za kufikia jamii zinasaidia jamii kuondoa magonjwa yanayowakabili wananchi hasa wanaoshindwa kuenda katika vituo vya afya kupata matibabu.
Baadhi ya wananchi wa walinufaika na huduma hizo wameishukuru taasisi hizo kwa kujitolea na kuwahudumia bila ya malipo yoyote huku viongozi wa mkoa huo walishiriki kuwahamasisha wananchi.