WANANCHI WAMESHAURIWA KUJITOKEZA KATIKA KUTOA TAARIFA JUU YA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

 

 

Wananchi wa mkoa wa kusini unguja wameshauriwa kujitokeza katika kutoa taarifa juu ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao juu ya utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Ushauri huo umetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja makarani khamis ahmed, wakati akizungumza na wananchi huko makunduchi kupitia mpango wake wa kusikiliza kero za wananchi kwa kupitia mobile polisi.Amesema iwapo wananchi watakuwa wepesi katika kutoa taarifa ya makosa kwa watendaji wa jeshi hilo, kwani itasaidia kujitathmini kiutendaji na kuwatambua watendaji wasio waaminifu katika jeshi hilo, ili  kuchukuliwa hatua za kisheria   Sheha wa shehia ya mtende khamis ramadhan amesema kuanzishwa kwa mpango wa mobile polisi litaliwezesha jeshi la polisi la mkoa huo  kujua matatizo ya wananchi kwa urahisi na kuweza kuchukuliwa hatua.Wakitoa  maoni yao mbele ya kamanda huyo ,wananchi hao wameliomba jeshi la polisi kusimamia vizuri suala la madawa ya kulevya na  kuondoka katika mkoa huo ambapo wameshauri kuchomwa moto pindi yanapokamatwa  ili kuinusu jamii katika janga hilo.