WANANCHI WAMESISITIZWA KUJENGA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

Wananchi wamesisitizwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini matatizo yanayowakabli kiafya na kuyatafutia matibabu.
Akizungumza katika zoezi la utoaji wa elimu ya afya na na meno pamoja na matibabu yaliofanyika katika kituo cha afya raha leo mkurugenzi kinga na elimu ya afya dk fadhil abadalla moh’d amesema wananchi wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao hadi tatizo linmopojikeza hali ambayo husababisha mrundikano wa maradhi.
Amewataka wananchi kuitumia fursa ya kila wanapokuja madaktari na kujitolea kusaidia afya ya jamiii kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa m atibu.
Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno kutoka tanzania bi lorino corneiro amesema hali ya afya ya kinywa na meno kwa tanzania ni kubwa kutokana na wanachi kukuosa elimu ya afya ya kinywa na meno na kusababisha ubovu wa meno.
Baadhi ya wananchi walofika kupatiwa matibabu wamesema kwa kiasi kikubwa wamefarijika kwa kuwafikia madaktari hao ku2wapatia matibabbu bure na kuomba madaktari wengine kuiga mfano huo ili kujenga afya imara kwa wananchi.
Zoezi hilo limeandaliwa na chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno kutoka tanzania bara wakishirikiana na madktari kutoka zanzibar ambapo zaidi zaidi ya wagonjwa 100 wamenufaika na huduma hiyo.