WANANCHI WAMETAKIWA KUTOFUMBIA MACHO MATENDO YA UDHALILISHAJI AMBAYO YAMEKUWA YAKIONGEZEKA KILA KUKICHA .

Wananchi wametakiwa kutofumbia macho matendo ya udhalilishaji ambayo yamekuwa yakiongezeka kila kukicha hapa nchini.
Akizungumza katika kongamano la udhalilishaji katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali , bi khadija bakari amesema kutokana na kukithiri uovu huo lazima kila mwananchi awe askari wa kupambana nayo.
Amesema wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa kwa kubakwa ,kulawitiwa na kubebeshwa mimba za umri mdogo huku baadhi ya wananchi wakikaa kimya.
Washiriki wa kongamano hilo wameelezea jinsi wanavyokerwa na vitendo hivyo kwani vimekuwa vikiwajengea hofu wakati wanapokuwa katika shughuli zao mbali mbali