WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO ZA KUPATA ELIMU YA KILIMO CHA KISASA

 

Wananchi wametakiwa kutumia fursa zilizopo za kupata elimu ya kilimo cha kisasa ili kuwa na udhalishaji mzuri utakaopelekea  kuwa na soko la uhakika.

Akizindua mafunzo ya kuwajengea uwezo  vijana na wazee wa wilaya ya kati  mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kati  mohamedi salum amesema ni wajibu wa wananchi  wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa kama hizi za elimu  zinapotokea  ili kwenda sambamba na azma ya serikali kuwa na uchumi wa viwanda

Amesema halmashauri ya wilaya ya kati  ipo katika mikakati ya  kuhakikisha  inaanzisha viwanda  ili kuwasaida wakulima na wafugaji kupata soko la bidhaa zao

Fidelis daniel  ni mkurugenzi wa kampuni ya kuwawezesha vijana na wananchi anaeleza lengo lao la kuanziasha mafunzo hayo

Nao baadhi ya wananchi na wakulima waaliopatiwa mafunzo hayo  wameelezea kuwa tatizo la ukosefu wa elimu na masoko ya uhakika limekuwa likirudisha nyuma juhudi zao  za mafanikio

Jumla ya washiriki 150  wakiwemo wakulima na wafugaji wa mazao ya nchi kavu na baharini wamepatiwa mafunzo hayo