WANANCHI WAMEWATAKA VIONGOZI WAO KUWASAIDIA KATIKA VIKUNDI WALIVYO VIANZINSHA

 

Wananchi wa shehia ya shauri moyo wamewataka  viongozi wao wa jimbo  kuwasaidia katika  vikundi walivyo vianzinsha  kwa lengo la kujikwamua na umasikini na kuachana na utegemezi.Wakizungumza na  baadhi ya watendaji wa mazingira walipowatembelea na kujua kazi zao wanazozifanya juu ya  utengenezaji wa  mbolea  kwa kutumia   taka  tafauti  za majumbani, lakini wanakabiliwa ukosefu vitendea kazi vya kuchukulia taka hizo.

Mkurugenzi wa  baraza la  manispaa  mjini aboud hasan  serenge, amesema  licha ya  kujikwamua na umasikini   kwa baadhi  ya wananchi wa shauri moyo  lakini  wameweza kuweka  mazingira safi na kujiepusha na uwezekano wa kutokea maradhi ya mripuko.Jumla ya  nyumba  200 zimenufaika na  mradi wa ukusanyaji    taka ambapo  ya  zaidi ya  wananchi  70 wameweza kujiweka pamoja na kunufaika  na mradi huo, ambapo kwa hatua ya awali wameanza na kupanda mboga mboga.