WANANCHI WANAOTAKA KUFANYA KAZI ZA UJASIRIAMALI KUZINGATIA UPATIKANAJI WA MALIGHAFI

 

Naibu waziri wa biashara na viwanda mhe, hassan khafidh  amewataka wananchi wanaotaka kufanya kazi za ujasiriamali kuzingatia upatikanaji wa malighafi,mashine na masoko kabla ya kuanza shughui hizo.Amesema wajasiriamali wengi nchini wamekuwa hawapati mafanikio ya kazi walizonzianzisha kwa sababu ya  kutozingatia mambo hayo jambo ambalo husababisha kufeli njiani na kupata hasara.

Akifunguwa mafunzo ya wajasiriamali wa mikoa mikoa mitatu ya unguja katika ukumbi wa skuli ya mwanakwerekwe ‘c’ mjini zanzibar hafidh  amewapongeza watu walioamua kuwa wajasiriamali kwa kusema wamefanya ujasiri wa kutaka kujikomboa na umasikini.Naibu waziri huyo ambae hotuba yake imesemwa na mkurugenzi wa biashara katika wizara hiyo ndugu saleh suleiman hamad amesema serikali ya mapinduzi zanzibar itaendelea kuwasaidia wananchi wanaojituma kwa shughuli za kujinasua na umasikini kwa kuwapa mafunzo na mikopo ili kuwa na mitaji ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.Mkurugenzi wa jumuiya ya zedo ndugu simai said suleian amesema jumuiya yake imejikita katika suala la kuondoa umasikini linaloikabili jamii hasa vijana ili kuwakinga wasijiingize katika mtengo wa kufanya mambo maovu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Akifunguwa mafunzo ya wajasiriamali wa mikoa mikoa mitatu ya unguja katika ukumbi wa skuli ya mwanakwerekwe ‘c’ mjini zanzibar hafidh  amewapongeza watu walioamua kuwa wajasiriamali kwa kusema wamefanya ujasiri wa kutaka kujikomboa na umasikini.

Naibu waziri huyo ambae hotuba yake imesemwa na mkurugenzi wa biashara katika wizara hiyo ndugu saleh suleiman hamad amesema serikali ya mapinduzi zanzibar itaendelea kuwasaidia wananchi wanaojituma kwa shughuli za kujinasua na umasikini kwa kuwapa mafunzo na mikopo ili kuwa na mitaji ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Mkurugenzi wa jumuiya ya zedo ndugu simai said suleian amesema jumuiya yake imejikita katika suala la kuondoa umasikini linaloikabili jamii hasa vijana ili kuwakinga wasijiingize katika mtengo wa kufanya mambo maovu.