WANANCHI WAZIDI KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA KULETA MAENDELEO

 

Waziri wa nchi  afisi ya  makamu wa pili wa rais mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed amewataka wananchi wazidi kujenga umoja na mshikamano katika kuleta maendeleo kwani ndio dhamira halisi ya mapinduzi ya zanzibar.

Mh. Aboud amesema hayo huko Sizini Wilaya ya Micheweni wakati akiweka jiwe la msingi la kituo cha Afya Sizini ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema Mapinduzi yamekuja kwa nia ya kumkombooa  Mzanzibar ili aweze kujitawala wenyewe na kujipangia mambo yao wenyewe.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mh. Harous Said Suleiman  amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi kwa busara zake za kuwaunganisha wazanmzibar.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar   Halima  Mauli amesema kituo hicho  cha sizini kitakapo kamilika kitatoa huduma zote ikiwa ni pamoja na huduma za akina mama  kujifungua.