WANANCHI ZIMBABWE WANA WASIWASI KUHUSU MUSTAKABALI WA NCHI YAO

 

 

Wananchi wa zimbabwe wana wasiwasi kuhusu mustakabali wa nchi yao baada ya rais wao robert mugabe anayezidi kutengwa kukataa kujiuzulu.

Mugabe ambaye jana alitarajiwa kujiuzulu kupitia hotuba yake aliyoitowa kwa taifa kupitia televisheni lakini badala yake hakujiuzulu.

Chama tawala cha zanu pf kimemtaka rais huyo ajiuzulu  leo au atakabiliwa na hatua za kumuondoa kwa nguvu madarakani.

Wanaharakati wa upinzani wamepanga kufanya maandamano zaidi kumshinikiza mugabe kuachia ngazi.

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa chama tawala wanasema mchakato wa kumuondoa madarakani mugabe huenda usifanikiwe kwa haraka na unaweza kuchukua siku kadhaa kukamilika.

Mugabe amepokonywa uongozi wa chama hicho lakini katika hotuba yake jana amesisitiza kwamba ataongoza mkutano mkuu wa chama hicho katikati ya mwezi ujao wa desemba.

Kwa sasa bado hatima ya mugabe kama kiongozi ni ya kutatanisha