WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WATACHUKULIWA HATUA

 

 

Mwenyekiti wa ccm taifa rais john pombe magufuli amesema ccm haitakubali uchaguzi wa chama uharibiwe na viongozi wanaojihusisha na rushwa na watakaobainika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akifungua mkutano mkuu maalum wa ccm mjini dodoma amesema chama hicho hakitapitisha viongozi wa aina hiyo kwa vile wanaweza wakakitia dosari chama hicho.

Amewataka wajumbe kufanya maamuzi ya busara katika mapendekezo yatakayotolewa kwa mustakabali wa chama na maendeleo ya taifa.

Akizungumzia utekelezaji wa ilani ya ccm mwenyekiti huyo amesema licha ya kufanikiwa katika kutekeleza masuala muhimu amesema suala la umasikini na ajira vinahitaji mbinu endelevu kukabiliana navyo ili kumarisha mazingira ya viwanda kutokanana na mchango wake kwa uchumi wa nchi.

Akitolea ufafanuzi agenda za mkutano huo katibu mkuu wa ccm abrahman kinana amesema mageuzi yanayoendelea kufanyika ndani ya chama si kitu kigeni na ni matakwa ya wanachama katika kujitathmini kufuatia chaguzi mbali mbali ambayo lengo ni kuendelea kukijengea imani zaidi.

Nae makamu mwenyekiti wa ccm zanzibar dk. Ali mohamed shein amesisitiza wanachama kuheshimu katiba ambayo ni muongozo wa kutekeleza ilani ya chama hicho.

Katika mkutano huo dk. Magufuli amependekeza majina ya nafasi ya naibu katibu mkuu ccm zanzibar kuwa abdalla juma mabodi, idara ya organization katibu amependekezwa kuwa perera ame silima na frank george haule katibu uchumi na fedha wa ccm.