WANAOVUKA KUACHA KUJAZANA KUEPUSHA AJALI

 

Wakaazi  wanaovuka kutoka tumbatu kwenda mkokotoni wametakiwa kuacha kujazana katika vyombo wakiwa ni familia moja ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo ajali.

Mkurugenzi mtendaji wa kamisheni ya kukabiliana na maafa seif shaaban  akiwa katika ziara ya kushtuliza katik abandari ya mkokotoni kukagua  vyombo vya usafiri vinavyovusha watu na mizigo katika bandari hiyo mesema kumekuwa na tabia ya watu wa familia moja kusafiri kwa chombo kimoja hali inayoweza kulet amaafa makubwa isipozingatiwa.

Aidha, mkurugenzi huyo amewataka wamiliki na manahodha wa vyombo hivyo kufuata sheria za usajili wa vyombo na kuacha tabia ya kupakia abiria kwa vyombo ambavyo leseni yake inaonesha vimeruhusiwa kupakia mizigo tu.

Nae nahodha wa chombo cha manaa kilichosajiliwa kupakia mizigo  mohamed simai ameiomba serikali kupitia mamlaka ya usafiri baharini kuwasaidia kuwapatia vifaa muhimu vya uokozi vitakavyowasaidia pindi hali ya dharura itakapotokea.

Kwa upande wa wananchi kutoka kisiwa cha tumbatu wameiomba mamlaka ya usafiri baharini kuwashauri manahodha kutoa chombo zaidi ya kimoja wakati wa kuvuka ili kuepusha msongamano wa watu wengi kupanda ndani ya chombo kimoja.

Afisa  kitengo cha operesheni na huduma za kibinadamu  kutoka kamisheni ya maafa makame khatib makame amewataka manahodha wa vyombo hivyo kuzingatia masuala ya usalama wa abiria na mali wakati wote wa safari.