WANASHERIA KUPATIWA UTAALAMU WA KUTAMBUA MAJERAHA YALIYOSABABISHWA NA KUSHAMBULIWA KWA RISASI

 

Utaalamu wa kutambua majeraha yaliyosababishwa na tuikio kushambuliwa kwa risasi au vilipuzi utaweza kuwasaidia wanasheria na waendesha mashtaka katika kukamilisha shauri ambalo linahitaji kusikilizwa mahakamani.

Akitoa taaluma ya ukusanyaji wa vielelezo vya silaha na vilipuzi kwa majeraha ya risasi ambayo yanahitaji kufanyiwa uchunguzi pamoja na vilipuzi, kwa wanasheria na waendesha mashataka wa serikali, maafisa upelelezi wa polisi pamoja na madaktari, mrakibu msaidizi wa polisi asp john mayunga sangija, taaluma hiyo ni muhimu katika kufanikisha majukumu yao ya kazi.

Taaluma nyengine iliyoyolewa kwa watendaji hao ni namna kufanya uchunguzi kwa watu wanaofariki kwa vifo vya kutatanisha na hata wanaofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wakati wanapohitaji huduma hasa katika viyuo vya afya na hospitali, taaluma hiyo imetolewa na dkt ahmed makata mwinyimtwana.