WANASHERIA WAMESISITIZWA WASIWE RAHISI KUTUMIWA

Wanasheria wanaoshuhulikia usuluhishi wa migogoro wamesisitizwa wasiwe rahisi kutumiwa na wadai na wadaiwa na kuegemea upande mmoja na kuhakikisha wanatenda haki kwa wote.
Naibu mwanasheria mkuu zanzibar mzee ali haji ameeleza hayo wakati akifunga mafunzo kwa wanasheria wasuluhishi wa migogoro huko marubi.
Amesema mafunzo hayo yawe ni chachu ya kuleta mabadiliko katika kusimamia haki kwa wananchi na yaweze kuleta tija kwa serikali na ni hatua moja wapo ya kufikia maendeleo.
Mkufunzi kutokia mahakama kuu daaresalaam masumbuko lamwai amesema ana matumaini makubwa ya kwamba malalamiko mengi ya wadai na wadaiwa yatafikia malengo endapo watayafanyia kazi mafunzo waliopatiwa.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa yamewawaongezea uwelewa wa kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu wa hali ya juu na kwamba yatawasaidia kuweza kutatua migogoro kwa haraka na kwa wakati .