WANAUME WAWILI WALIOFANYA SHAMBULIO LONDON

Polisi nchini uingereza imewataja wanaume wawili kati ya watatu waliofanya shambulio katika eneo la london bridge na kuwauwa watu saba kabla ya kuuawa kwa risasi.
Kitengo cha usalama uingereza kimemtambua mmoja wao kuwa ni khuram butt ambae aliwahi kuonekana kwenye kipindi cha televisheni mwaka jana kilichoangazia kundi lenye itikadi kali linalounga mkono islamic state .
Wote waliokuwa wamekamatwa na polisi kufuatia mauaji hayo wameachiliwa bila mashtaka.