WANAUSHIRIKA WAMEIYOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA MASOKO YA KUUZA BIDHAA ZAO

 

 

Wanaushirika  wa kikundi cha mungu tupe kheri  cha  donge mjimbi wameiyomba serikali kuwatafutia masoko ya kuuza bidhaa zao kwani wamekuwa wakipata hasara ya bidhaa  wanazo zalisha  kuharibika.Wakizunguza na zbc kwa nyakati tofauti wananchi hao  wamesema ili waweze kujikidhi katika maisha yao njia pekee ni kupata soko maalum la kuuza bidhaa hizo.

Wamesema  kikundi hicho kimekuwa kikijishuhulisha na uwatikanaji wa miche ya mazao mbali mbali pamoja  na kujishughulisha na ushoni lakini wamekuwa na changamoto kubwa ya kukosa wateja wa kununu bidhaa hizo.Kikundi  hicho  ambacho  kinawanachama  30 wakiwemo wanawake na wanaume wamekuwa wakijishulisha na miradi mabli mbali ya kuendeleza maisha yao pamoja na familia zao.