WANAWAKE KUFUATA MILA NA SILKA NA DESTURI ZA MAZANZIBARI IKIWEMO KUJISTIRI.

 

Waziri wa Biashara na Viwanda Mh Amina Salum Ali  amewataka wanawake kukuata ma silka na desturi za mazanzibari ikiwemo kujistiri.

Amesema mwanamke pindipo atakapo jistiri heshma yake itaheshimika popote pale Duniani.

Akizungumza katika sherehe ya kusherehekea siku ya Mwanamke Duniani na vazi la Hijabu Beach  Resort  Waziri Amina amesema ili mwanamke atambulike ni vyema wanawake wakajiingiza katika mambo ya kiuchumi ili kukuza biashar na heshima kwa wanawake wote.

Akigusia maendeleo ya wanawake yaliopatikana  miaka hii ni makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa kisiasa biashara.

Mdau wa pink Hijabu do tor Mariam khalfan amesema vazi la Hijabu limezungumziwa katika dini zote ikiwemo mwanamke kujistiri.

Mtunza nidhamu kutoka Zanzibar Lishe Shangwe Yussuf amesema lengo lakufanya sherehe hiyo nikumfanya mwanamke atambulike kwa heshima zaidi.

katika ghafla hiyo vyeti mbali mbali vilitolewa.pamoja na harambee iliyochezeshwa na Naibu spika mh mgeni juma pamoja na maonyesho ya wajasiri amali.