WANAWAKE NA WATOTO BADO WANAHITAJI KUHAMASISHWA

 

 

Mwakilishi mkaazi wa shirika la kusaidia watoto ulimwenguni save the children fund anaemaliza muda wake zanzibar bi. Mali nelson amesema wanawake na watoto bado wanahitaji kuhamasishwa ili kuweza kubadili tabia itakayopelekea kupatikana ustawi kwao na jamii

Akizungumza katika hafla ya kuagana na uongozi  wa wizara  ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto bi mali amesema kwa kufanya hivyo wizara pamoja na taasisi nyengine zitakuwa zimetekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Amewapongeza viongozi hao kwa ushirikiano waliompa wakati wote akiwa zanzibar ambao umemuwezesha kutekeleza majukumu yake.

Nae katibu mkuu wa wizara hiyo bi.fatma gharib bilali  amempongeza  mwakilishi huyo kwa kuwa karibu na wizara hiyo na kwamba serikali ya mapinduzi zanzibar inathamini mchango unaotolewa na shirika hilo la save the children fund.

Wakati huohuo katibu mkuu huyo amelitaka  baraza la vijana kujipanga vizuri katika shughuli zake ili kufikia malengo wakati alipokutana na sekretarieti ya baraza  hilo kuzungumzia utendaji kazi wa baraza hilo.