WANAWAKE NCHINI WAMEHIMIZWA KUJIENDELEZA

 

 

Wanawake nchini wamehimizwa kujiendeleza,kujituma na kutojiweka nyuma   katika  suala  zima  la kukuza uchumi  na kuondokana na umaskini.

Mratibu wa mradi wa kuhamasisha wanawake  kujiunga  na utembezaji watalii nd anisa juma ametoa kauli hiyo katika kikao kilichoandaliwa na  kituo   cha  kawa traning center kiliopo kiponda  chenye lengo la kutoa uelewa juu ya  kituo hicho  nakuweza kuwapa mwamko wanawake  katika kujiunga   ili wanufaike  na  suala la   kujiamini  na  hatimae kujiajiri .

Nae   mkurugenzi  wa  kituo  cha  kawa  traning center   suzan deglin  amesema  lengo  la  kuanzisha  kwa  kituo  hicho  kwa  vijana  ni  kutaka  kuwaendeleza  kitaaluma   katika  fani tofauti  ikiwemo  utembezaji  watalii,na  kuwataka  kanawake  kuitumia  fursa  hiyo  kwani ni moja  ya  ajira  itakayompatia  kipato  na  kuachana  na fikira  za   kuwa  kazi  hiyo  ni  kwa wanaume  pekee.

Wakitoa  `maoni yao  juu ya  mwamko mdogo wa wanawake  katika kujiunga  na  fani  hiyo baadhi ya   washiriki wa  kikao hicho  wameshauri   kutolewa  elimu  zaidi kwa  jamii  kuhusu umuhimu wake  ili  wapate  kuzitumia fursa  kama  hizo.

Kawa  traning  center   ni  kituo  chenye  kutoa  taaluma   ya  utembezaji watalii, kinadharia  na  vitendo  ambacho  tayari  kimeshatoa  wahitimu  tisini tokea kuanzishwa kwake mwaka 2011.