WANAWAKE TISA WAMEAMUA KUANZISHA MRADI WA KUJIAJIRI WENYEWE

 

Kikundi cha wanawake tisa katika maeneo  ya mwera mtofaani wameamua kuanzisha mradi wa kujiajiri wenyewe baada ya kuona  hawana ajira wakati walipomaliza masomo yao ya kidato cha nne.

Wanawake hao wamejiingiza  katika fani ya ushoni, ufumaji pamoja na uchoraji baada ya kushawishiana   ili kuacha kazi za utegemezi  ndani ya familia zao.

Wakizungumza na habari za biashara wamesema wameamua kujikusanya pamoja baada ya  kumaliza masomo ya  sekondari huku wakiwa hawana uwezo wa kujiendelea  na elimu ya juu.

Wamesema mbali na kazi zao hizo  pia wanawake hao wamefanikiwa kuanzisha mradi mwengine wa biashara ya kuuza mabaibui na kukopesha kanga baada ya kufanikiwa kupata  mtaji wa kutosha katika kikundi chao.

Hata hivyo  wajasiriamali hao wamewashauri  wanawake wengine kutokukata tamaa  ya kutafuta na sio kuwategemea wanaume pekee.