WANAWAKE WAMETAKIWA KULICHUKULIA KWA UZITO SUALA LA KUCHUNGUZA AFYA MAPEMA

 

Wanawake nchini wametakiwa kulichukulia kwa uzito unaostahili suala la kuchunguza afya mapema hasa kuhusiana na maradhi ya wanawake ikiwemo uvimbe katika tumbo.Imebainika kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanasumbuliwa na tatizo hilo lakini kuchelewa kujigundua hadi kufikia hatua kubwa inaweza kuwaletea madhara mbalimbali ikiwemo kukosa uzazi na hata kuharibika kwa mimba.

Daktari kutoka hospitali ya tasakhtaa (global) ambae ametoa elimu ya afya kwa wananchi mbali mbali iliyoambatana na zoezi la kupima afya bure kwa muda wa siku nne amesema njia muhimu kwa akina mama ni kujenga tabia ya kucunguza afya mara kwa mara ili kubaini tatizo katika hatua ya awali.Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema fursa hiyo ya kupata elimu pamoja na uchunguzi wa afya inawapa muamko wa kuju afya zao huku wakiiomba jamii kuacha kukimbilia kwenye tiba za kienyeji kwani zinaweza kuwongezea madhara.Afisa uhusiano na huduma wa hospitali hiyo bi victoria mwakanjuki amesema muitikio wa wananchi umekuwa mzuri na watahakikisha wanaifikia jamii ya vijijini katika kuelimisha masuala ya afya.