WANAWAKE WANA NAFASI KUBWA YA KUCHANGIA MABADILIKO

 

wanawake wana nafasi kubwa ya kuchangia mabadiliko muhimu  katika jamii iwapo watashirikishwa ipasavyo katika vikao vya kufanya maamuzi katika masuala ya kimaedneleo hapa visiwani

akiwasilisha mada inayohusu sheria na haki za wanawake na watoto katika muendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kamati za shehia za kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ,mwanasheria kutoka wizara ya kazi ,uwezeshaji ,wazee ,wanawake na watoto didas khalfan amesema kumshirikisha mwanamke kutoa maamuzi ni sawa na kuishirikisha jamiii nzima.

didas ameendelea kubainisha kuwa licha ya kuwepo harakati na mikakati ya kupambana na vitendo viovu bado wanawake na watoto wapo katika hatari ya kupatwa na mikasa hiyo kutokana na maumbile na mazingira yao .

akizungumza katika mkutano huo sheha wa shehia ya bambi amour pandu mkombe ameeleza kuwa yapo mafanikio katika harakati za kupambana na ukatili na udhalilishaji lakini bado baadhi bya wazazi wa hawatoi mashirikiano ya kutosha kuviwezesha vyombo vya sheria kutoa maamuzi sahihi .

baadhi ya washiriki wamesema elimu hiyo ni muhimu katika kusimamia harakati zao za kupinga vitendo vya udhalilishaji na kubainisha kuwa mashirikiano ya pamoja ndio njia pekee itakayoweza kuondoa tatizo hilo hapa nchini .

lengo la mpango kazi mpya wa mwaka 2017/2022 ni kutoa mkusukumo kwa watendaji ya shehia katika kuibua na kuchukua hatua zitakazoweza kuondoa kabisa udhalilishaji zanzibar .