WANAWAKE WANAOJISHUGHULISHA NA KAZI ZA UJASIRIAMALI

 

Wanawake wanaojishughulisha na kazi za ujasiriamali nchini wametakiwa kuitumia wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto kwa kupata mikopo nafuu itakayowawezesha kukuza uchumi wao.

Wito huo umetolewa na mke wa Rais wa Zanzibar mama mwanamwema shein wakati  akizungumza na wanakikundi cha ushirika cha siri moyoni cha kiliopo Unguja ukuu na kusisitiza umuhimu wa kuitumia wizara hiyo itawapa fursa za kuendeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na uzalishaji.

Katika ziara hiyo ya mama shein alieyofuatana mke wa balozi mdogo wa china aliopo Zazibar Bi liu xiu ambapo kamera ya habari za biashara na uchumi ilishuhudia wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanakikundi hicho na kutoa misaada wa vyarahani na fedha taslim.

Nae mke wa balozi mdogo  wa China Bi liu xiu amesifu juhudi za wajasiriamali hao kwa kumpambana na umasikini kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali na  kuahidi kuongeza ushirikiano kati ya china na Zanzibar.

Katika risala ya wana vikundi hao wameishukuru Serikali kwa juhudi za kuviwezesha vikundi mabimbali nchini na kuomba  kuzipatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili.