WAOKOAJI WANAENDELEA NA KAZI YA UOKOZI KATIKA MAENEO YALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Waokoaji wanaendelea na kazi ya uokozi katika maeneo yaliokumbwa na mafuriko kusini/mashariki mwa texas ambako watu wamekwama kutokana maafa ya kimbunga harvey.
Wakati juhudi hizo zikifanyika rais donald trump ameliomba bunge la marekani kuidhinisha kiasi cha dola bilioni 7 ili kukabiliana na maafa.
kimbunga hicho kinachotajwa kuwa ni kibaya zaidi nchini marekani kimesbabisha watu zaidi ya milioni moja kukosa makaazi huku kukiwa na hofu ya wengine 50 kupoteza maisha kutokana na mafuriko katika mji wa houston jimbo la texas.