WAPALESTINA WAKATAA HATUA MPYA ZA ISRAEL MJINI JERUSALEM

Kiongozi wa palestina mahmoud abbas anasema kuwa ataendelea kukata mawasiliano na israeli licha ya kuondolewa kwa mitambo ya kutambua chuma eneo takatifu mashariki mwa jerusalem.
Kuwekwa kwa mitambo hiyo kulisabaisha ghasia kwa wapalestina ambao waliiona kama hatua ya israel kutaka kudhibiti eneo hilo.
Rais wa palestina abbas na kiongozi wa kiislamu ambaye anasimamia eneo hilo, walitupilia mbali mabadiliko hayo.