WAPIGANAJI 40 WA NJE WANAOUNGA MKONO UTAWALA WA SYRIA

 

Takriban wapiganaji 40 wa nje wanaounga mkono utawala wa syria wameuwawa katika shambulizi la mabomu jana usiku lililofanywa karibu na eneo la al-hari, mashariki mwa mpaka na iraq.

Kulingana na shirika la uangalizi la syria lenye makao yake nchini uingereza shambulizi hilo lilikuwa miongoni mwa mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya majeshi yanayounga mkono serikali ya syria.

Vyombo vya habari vya serikali ya syria viliripoti kuhusu shambulizi hilo vikinukuu vyanzo vya kijeshi huku likiulaumu muungano wa majeshi unaoongozwa na marekani unaopambana na kundi la wanamgambo linalojiita dola la kiislamu, is, kwa kufanya shambulizi hilo.

Muungano huo hata hivyo haukuzungumzia lolote juu ya shambulio hilo na shirika hilo la uangalizi halikuweza kutambua mara moja ni nani aliyehusika na shambulizi hilo la al-hari.