WARUSI YAMKUMBUKA KIONGOZI WA UPINZANI BORIS NEMTSOV

 

WATU WAPATAO KUMI NA TANO ELFU WAMEANDAMANA MJINI MKUU WA URUSI, MOSCOW KUOMBOLEZA MWAKA WA PILI TOKEA ALIPOULIWA KIONGOZI WA UPINZANI BORIS NEMTSOV.

MAANDAMANO MENGINE KADHAA YAMEFANYIKA KATIKA SEHEMU TOFAUTI NCHINI HUMO, HUKU FAMILIA YA BW: NEMTSOV IKIILAUMU SERIKALI KWA KUTOFANYA UCHUNGUZI WA KUTOSHA KWA KUZINGATIA CHUKI ZA KISIASA.

NEMTSOV NI KIONGOZI WA NGAZI YA JUU KUWAHI KUUAWA TOKEA RAIS VLADIMIR PUTI AINGIE MADARAKANI.

WAKATI HUO HUO, MAREKANI IMEIKOSOA URUSI KUHUSU VUGUVUGU ZA MAPIGANO NCHINI UKARINE AMBAPO IMEITAKA URUSI KUHESHEMU MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPIGANO, BAADA YA IDADI YA MAUAJI MIONGONI MWA WANAJESHI WA UKRAINE KUONGEZEKA.