WASANII WA KIZAZI KIPYA WAMETAKIWA KUZITUMIA FURSA MBALI MBALI WANAZOZIPATA

 

Bodi ya wazee ya kamati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya imewataka wasanii kuzitumia fursa za sherehe na matukio mbali mbali kwa ajili ya kujipatia kipato.

Akizungumza katika kikao cha wazee wa bodi kamati tendaji ya chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika ukumbi wa sanaa rahaleo , omar yussuf chunda amesema kuna fursa nyingi kwa wasaniii wakizitumia vyema kwani wana nafasi kubwa ya kuitangaza nchi.

Kwa upande wao wasanii wa muziki wa kizazi kipya zanzibar wamesema wapo katika jitihada za kuifahamisha jamii kuijua thamani yao ambapo wamewataka wazanzibar kuthamini vitu vya kwao wakiwemo wao wasanii wa zanzibar.

Baada ya wasanii hao kusema hawapewi nafasi kubwa sana katika matukio mbali mbali na badala yake wasanii kutoka nje ya zanzibar wanapewa kipaombele kuliko wao, nimemtafuta  katibu mtendaji baraza la sanaa sensa ya filamu na utamaduni dk omar abdallah adam kujibu malalamiko hayo.