WASANII WAKONGWE WA TAARAB WAELEZEA FARAJA YAO YA KUPATA KIFUTA JASHO

 

Wasanii wakongwe nchini katika tasnia ya muziki wa taarab asilia waliotamba na vikundi mbalimbali vya sanaa hapa zanzibar wameelezea faraja yao ya kupata kifuta jasho kutokana na mchango wao katika kazi hiyo ya sanaa.

Wasanii hao ambao wametembelewa na ofisi ya haki miliki ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kuwapa mirabaha inayotokana na matumizi ya kazi zao katika shughuli mbalimbali ikiwemo kwenye vyombo vya habari wamesema, walitumia muda mwingi kujitolea katika kazi hiyo na kitendo cha kupata mafao hayo kinawapa imani kuwa bado wanakumbukwa.

Miongoni mwa wasanii waliotembelewa ni pamoja mzee mwinyiwesa idarous mtunzi wa nyimbo, bi fatma issa juma, mwanacha hassan kijore, bi njiwa na bi mwajuma ali hassan aliyeimba nyimbo ya mpunga.