WASHIRIKA WA MAREKANI WAMEPONGEZA HATUA YA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA

Washirika wa marekani, asia wamepongeza hatua ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo vipya korea kaskazini kwa kufanya jaribio la sita la silaha za nyuklia hatua ambayo imepingwa vikali na nchi hiyo .
Baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, japan na korea kusini zimesema ziko tayari kuishinikiza zaidi korea kaskazini iwapo nchi hiyo itakataa kukomesha mpango wake hatari wa silaha za kinyuklia na kurusha makombora.
Azimio hilo limepingwa na nchi za china na urusi ambazo zimeendelea na msimamo wake wa kutaka zaidi yafanyike mazungumzo kutatua mzozo huo kuliko vikwazo.
Vikwazo vilivyowekwa ni pamoja na mafuta na uuzaji wa makaa ya mawe nje ya nchi, madini ya risasi na vyakula vya baharini, uuzaji wa nguo za korea kaskazini nje ya nchi, kusitisha usafirishaji wa gesi asilia na kudhibiti usafirishaji wa bidhaa za mafuta.