WASHIRIKI 20 WA KUNDI LA VUNA KIPAJI WAMESAINI MKATABA WA KUFANYAKAZI ZA SANAA NA MAIGIZO ZBC

 

Jumla ya washiriki  20  wa kundi la vuna kipaji  wamesaini mkataba wa  kufanyakazi  za sanaa na maigizo na shirika la utangazaji  zbc  kwa muda wa mwaka mmoja.Hafla hiyo hiyo ya utiaji saini  mikataba hiyo   imefanyika  katika studio za zbc karume house na kuhudhuriwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji  zbc  bi, iman duwe ambaye amewasisitiza washiriki hao kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa katika  kufikia  malengo ya kuwa wasanii wazuri katika tasnia ya maigizo nchini .

Aidha pia amesema zbc itaendelea na mpango wake wa  kuibua vipaji mbalimbali na kuviendeleza ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya shirika la utangazaji na kuwawezesha washiriki kuonesha  vipaji vyao .Naye msimamizi mkuu wa washiriki hao katika kazi watakazozifanya na zbc  kuanzia sasa  mzee yusuf  amesema  atahakikisha washiriki hao wanafanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu na kuzingatia maadili ya kazi yao ili kufukia lengo husika

Naye mratibu wa shindano la vuna kipaji na zbc saleh abdalah amesema ni jambo la faraja kuona msimu wa kwanza wa shindano hilo umekuwa na manufaa makubwa  huku akiwaahidi wananchi wakae tayari na msimu wa pili wa vuna kipaji itakayowajia hivi karibuniNao  baadhi ya washiriki wa shindano hilo wameelezea matumaini yao mara baada ya kusaini mikataba na  shirika la utangazaji zbc